Tuesday, January 29, 2019

UTUMWA WA TAMADUNI ZA KIMAGARIBIU KWA AFRIKA HAUEPUKIKI KWASABABU YA UMASIKINI WETU


UMASIKINI UMETUGEUZA KUWA WATUMWA WA TAMADUNI ZA KIMAGARIBI. 


 USHOGA, USAGAJI, NDOA ZA JINSIA MOJA NA KUBADILI JINSIA (LGBT).



Usemi wa mjini, "Bosi Huwa hanunuwi hata siku moja"; unatambua wazi kwamba huna sehemu ya kulala unamtukana baba mwenye nyumba unategemea nini..?  Zamani utasikia mama ama Baba anakwambia utajua utakapokula leo maana unaonekana umekuwa siku hizi kisa tu hujafanya kazi uliyopewa au umegoma kuchota maji ama hujaenda kulima au hujafanya vile wazazi wanavyotaka sasa wanakwambia utafute utakapolala na utafute pia kwa kula basi hapo yatafata na maneno mengine makali juu yako.



Hivyo ndivyo mataifa masikini yanavyopata shida katika kutekeleza matakwa ya mataifa makubwa ukienda kinyume utapewa onyo na ukijifanya unaleta kiburi basi wanakata misaada mpaka ufate vile wanavyotaka wao tofauti na hapo ukubali kula nyasi na kuendesha nchi kwa jasho na msoto usio wa kawaida na hapa ndipo  tunakamilisha msemo unaosema BOSI HUWA HANUNIWI.  Kuna sehemu nyingine wako sahihi maana wanatunyooshea viongozi ambao wameshindwa kuongoza  nchi kwa kufuata Katiba ya nchi na kushindwa kuheshimu mikataba ya kimataifa ambayo wamekuwa wakisaini kuanzia mwaka 1945, 1946, 1948, 1976, 1980s na mpaka miaka ya 2000s .



Suala la Ushoga ni suala nyeti tena katika unyeti wake na ni suala la muda mrefu sana kulingana na Historia ya mwanadamu kwa maana kwamba hata kabla ya ujio wa Dini watu walikuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile (Same Sex Sexual).   Mambo yalikuwa yanafanyika hapo Mashariki ya kati ambako ndiyo chimbuko la mambo mengi sana. Baada tabia hiyo ilivyokuwa kubwa katika miji miwili ya kale sana yaani SODOMA na GOMORAH ndipo pale Mungu akatuma malaika wake na kuangamiza miji ile miwili kwa Moto na kufutilia mbali kizazi kile.  Lakini hata baada ya hapo jambo hili liliendelea kufanyika japo kwa siri kubwa sana miaka mingi baadae.



Baada ya miaka mingi kupita suala la Ushoga (Gaysim) lilikuwa linafanyika huko katika ngome za Uguriki (Anciant Greece)  lakini jambo hili lilikuwa linafanyika kwa siri sana tena katika majumba makubwa ya Kifalme.  Jambo hili lilikuwa linafanyika kwa Siri kubwa mno na wahusika wakubwa walikuwa watu wazito na maarufu. Ila kuna Sheria zilitengenezwa pia kwamba mtu akipatikana anafanya tendo hilo ambalo kwa sasa linajulikana kama (Homosexual) Basi Adhabu yake ilikuwa ni Kifo ama kunyongwa lakini adhabu hii ilitolewa kwa watu tabaka la chini na hata baada ya Utawala wa Ugiriki kupita zilifuata tawala zingine kama Roman Empire hata huko pia mambo haya yalikuwepo kwa kiasi fulani na yalipigwa vita sana ila yaliendelea kushamiri kadri siku zilivyokuwa zinazidi kuyoyoma.



Historia ya Ushoga ni ndefu sana kwa upande wa Marekani kwa ujumla wake mwaka 1513 Wafaransa na Waingereza walikuwa na Utamaduni wa kuwakamata RedIndians na kuwafanyisha mapenzi kinyume na maumbile kwa kuwatumia mbwa wao wa kivita yaani wanawakamata wahindi wekundu (Redindians) na kuwafunga Kamba alafu wanachukua mbwa tayari kwa kifanya nao tendo hilo kinyume na maumbile. Miaka ya 1600s mpaka mwaka 1700s Waingereza na Wafaransa walikuwa wanalazimisha wafungwa ama watumwa wao na kufanya nao mapenzi kinyume na maumbile na tabia hii iliendelea na kushamiri sana Marekani sana sana kwenye Kambi za kijeshi na kwenye Kambi za Watumwa kusini mwa majimbo ya Marekani na maeneo mengine.  Mwaka 1789 katika katiba ya Marekani waliruhusu mambo mengi ambayo kwa huku kwetu Afrika ni katazo japo miaka  imeenda wakaamua kuidhinisha na kuonekana ni jambo la kawaida na umekuwa utamaduni wao na sasa wanataka na mataifa mengine wafanya hivyo wakidai ni haki ya mtu kutumia mwili wake anavyotaka yeye.



Twende mbele kidogo waungwana mnamo mwaka 1967 Bunge la Uingereza walipitisha kifungu kwenye katiba yao kuruhusu ndoa ya jinsia moja (Gaysim & Lesbians) hivyo ni jambo la kawaida sana Uingereza na mataifa mengine mengi barani Ulaya na ndoa hizi zimekuwa zikifungwa Katika Makanisa Makubwa Barani Ulaya na inafanyika bonge la sherehe na huu ndiyo utamaduni wao na wanaofanya hivi ni viongozi wakubwa wa kiserikali na wamiliki wa makapampuni makubwa na viwanda katika taifa kama Uholanzi, Ujerumani, Poland, Swiden, Denmark, Lativia kuna idadi kubwa ya ndoa za jinsia moja na wale wanaofanya tendo la ndoa katika jinsia moja yaani Homosexual. Sasa hawa wanaofanya hivyo ndiyo wafadhili wakubwa wa Miradi mbalimbali katika Bara hili la Afrika na katika hilo hakuna ubishi yaani hawa ndiyo wanalifanya Bara la Afrika linapiga hatua kimaendeleo maana Mataifa mengi ya Afrika yanaongoza Nchi kwa kutegemea misaada. Umoja wa Afrika (AU) unategemea pesa kutoka Ulaya kwa takbani asilimia 70%.



Haya mambo ni mazito mno, haya mambo ni nyeti maana yana unyeti wake. Historia inaonyesha kwamba mwaka 1990 ndiyo mwaka pekee ambao mashoga walifikia mafanikio makubwa katika harakati zao za kutaka Serikali ya Marekani waruhusu kile walichokiita LGBT yaani Lesbians, Gaysm, Bisexual na Transgenda na kuanzia miaka hiyo LGBT iliruhusiwa lakini katika majimbo machache sana nchini. Mpaka kufika mwaka 1998 idadi ya wahusika iliongeza maradufu na kupata uungwaji mkono mkubwa sana kwa wanachama wa Jinsia moja yaani usagaji, ushoga, ndoa za jinsia moja, kubadilisha Jinsia. Marekani unaruhusiwa kubadili jinsia kutoka wa kike kwenda wa kiume au kutoka wa kiume kwenda wa kike kule unaruhusiwa (BE THAT YOU CAN BE).



Wanaharakati wa LGBT waliingia mtaani kuhamasisha watu wajitokeze kwa wingi ili kuunga mkono mambo yote hayo ambayo yametajwa hapo juu na kwa kuwa watu hawa wana ushawishi na wako kwenye nafasi za juu Serikalini na wengi wao ni watu maarufu na wenye pesa chafu hatimaye mnamo 26/06/ 2003 mahakama ya juu kabisa nchini Marekani (US Suprime Court)  ilihidhinisha suala la Ushoga, Usagaji, ndoa za Jinsia moja na kubalidilisha jinsia na mambo mengine katika majimbo 23 pekee. Kutokana Marekani kuunga mkono sakata hilo mashoga walianza kuongezeka kwa kasi ya ajabu. Ikafika wakati wakawa wanaruhusiwa kufanya hivyo mpaka makanisa  yakaruhusu ama kuhalalisha jambo husika na ndoa zinafungwa kama kawaida Makanisani na kwa kutumia uwezo wa taifa hilo kubwa Duniani wanataka kuona utamaduni huo unakubalika katika mataifa karibia yote Duniani kwa hiari ama kwa lazima kama unajiweza katika kila kitu pinga kama hujiwezi hunabudi kuungana nao.



Wajuvi na wadadavuaji wa mambo wanakwambia Amerika wanacheza karata yao vyema sana (Americans play the Cards Rights). Bado mambo yanaendelea, mwaka 2012 Rais wa 44 wa Marekani Bwa. Barack Obama aliwahi kusema kwamba Marekani ndiyo sehemu pekee Duniani kwamba kila kitu kinawezekana na sehemu pekee pia ambayo mtu anaweza akazifikia ndoto zake. Maneno haya ni mazito mnoo kwa mtu ambayo anajua kutafakari vema. Mnamo 26/06/2015 mahakama ya juu ya Marekani ikatoa kibali cha Kuruhusu LGBT katika majimbo yote 54 hivyo basi ushoga kwa ni kitu ambacho kimehalalishwa na wala hawaoni shida na mataifa yote Barani Ulaya na Canada suala la ushoga limeruhusiwa na wanataka kuona na mataifa mengine mnafuata utamaduni huo hakika na hawataki kuona mashoga wanaonenewa ama kunyanyaswa. Kufanya hivyo utawekewa vikwazo vya kichumi na Marekani ama Bara la Ulaya hutaingia Kamwe.



Vivyo hivyo katika mambo mengine wanakosea pale wanapoingilia tamaduni zetu na kutuamulia baadhi ya mambo japo hatuna budi kufuata maana tumekubali kuwa masikini na tumekubali kwamba bila misaada hatuendi popote. Mambo ya ushoga ni mambo mazito sana huwezi kuyatatua kwa kutaja watu pasipo msingi wowote lazima kama taifa likae chini na kutathimi nini kifanyike lakini siyo kwa kukurupuka sijajua ile operation imeishia wapi na je ni mashoga wangapi wamekatwa mpaka sasa japokuwa hatari yake ni kubwa mno. Mtu pekee aliyekuwa anaweza kukemea alikuwa ni Roberty Mugabe  lakini na yeye baada ya kutumia nguvu kubwa mpaka kuongea hayo Umoja wa Kimataifa kwa kupinga mambo ya Ushoga (Gaysim) aliishia kuwekawa vikwazo vizito vya kiuchumi (Economic Sunctions)  ambayo imeipelekea Zimbabwe kudhohofika kiuchumi  japo kuna sababu nyingine nyingi nyingine za Kisiasa, umasikini wetu unatufanya tushindwe kupinga ama kukemea hadharani ushetani wa Kimagharibi Kama Ushoga na Mambo mengine ya kushangaza.



Uganda mwaka 2015-2016 walitengeneza sheria kali sana dhidi ya mashoga na mpaka wakawa wanawauwa na kuwachoma moto  lakini wakubwa waliposikia  hakuna rangi waliacha kuona na mpaka sasa sheria ile waliifutilia mbali na sijui Uganda waliishia wapi na Operation yao ya kuwakamata na kupiga mawe mashoga kama mbwa mwitu au na wao ilkuwa ni mihemko tu. Madhara yake ni makubwa mnoo mpaka Leo Mseveni kwenda Marekani ni changamoto maana mara ya mwisho alitumuliwa akiwa hotelini nchini Marekani kisa alikuwa kinara wa kupinga ushoga Afrika. Mambo kama haya hayawezi kutatuliwa kwa matamko ama nguvu fulani lazima viongozi wa Bara la Afrika wakae na kuja na msimamo mmoja ambao utakuwa unatambulika na Umoja wa Kimataifa japo natambua jambo kama hili kutendeka ni ngumu Ila lazima Umoja wa Afrika (African Union)  usimame na kutoa tamko lakini kumuachia Makonda peke yake ni kumtoa kafara.



Kumuachia Mseven pekee yake pia ni kumtoa kafara kama alivyoachiwa Gabriel Roberty Mugabe pekee yake pia walimtoa kafara. Afrika waje na msimamo thabiti lakini siyo matamko na vitisho vya mtu mmoja mmoja maana matamko  haya yamejaa mihemko hayatasaidia maana haya mambo ni mazito sana hayafai kuyaendesha kisiasa. Mtu mmoja kusimama ni kama kumpigia kelele tembo ukitegemea hatakunywa maji. Tatizo linakuja kwamba viongozi wengi wa Bara la Afrika wanapoenda kwenye  Mataifa ya watu na kuambiwa wasaini mikataba wao wanasoma Kichwa cha Habari na kudondosha wino na linapotokea jambo wanaanza kupinga huku kifua mbele na wanasahau kwamba walisaini hicho wanachopinga na kukishangilia. Mikataba juu  ya kuheshimu haki za binadamu walisaini mwaka 1946, mwaka 1980s, mwaka 1970s, mwaka 1990s na mingineyo ilisainiwa miaka ya 2000s. Viongozi hawakuelewa maana ya Haki za Binadamu na endapo hawakuelewa basi hawana budi kurejea Mikataba mbalimbali iliyowahi kusainiwa. Hivyo kama viongozi lazima mtulize kichwa siyo kudandia dandia tu mambo wasiyokuwa na taarifa nayo.



Unajua Dunia inakwenda kwa kasi sana ambayo mengine hatupaswi kuendelea kuyakumbatia maana yamekwishapitwa na wakati yalikuwepo mambo mengi sana ya ajabu hapo awali kwa sasa yameonekana hayana maana yamekuja mengine mapya hivyo taifa lolote lile halipaswi kushindwa kwenda na mabadiliko haya makubwa japo mambo mengine kama ya ushoga haya ni paradox sana yalikuwepo tangu enzi na yameendelea kuwepo haya yanaoneka kutuzidi uwezo ila hakuna shida tuendele kupambana maana atakuja huyu atapalilia, atakuja yule anatavuna na mwingine atakula hivyo tulipofika siyo mbaya.