Monday, January 14, 2019

Mshahara ni Chanzo Cha Umasikini

Mshahara ni Chanzo Cha Umasikini

Imekuwa ni historia ya muda mrefu ambayo inazidi kuangamiza wengi kutoka kizazi hadi kizazi. Kinachosikitisha zaidi ni wachache ambao wanajua jambo hilo licha ya kuwa ni tatizo la muda mrefu. Watu wengi huhangaika kila kona namna ya kujinasua kiuchumi. Hata hivyo kundi la hawa wachache wanaojua tatizo bado wengine wanaendelea kuhangaika namna gani wataweza kujinasua katika tatizo hili, nalo si jingine ni Umasikini.  Wengine utasikia wakisema nimepata kazi na ninalipwa mshahara, swala siyo mshahara bali mshahara wako umekusaidiaje kujinasua na hilo tatizo. Kuwa na mshahara hakukufanyi kukwepa umasikini. Haijalishi kiwango cha mshahara mkubwa kiasi gani. Kumbuka  hakuna mshahara ambao umeweza kumtosheleza mtu duniani. Kumbuka kuzaliwa katika familia masikini si kosa bali kosa ni kufa masikini. Je kuzaliwa masikini ni lazima ufe masikini au kuzaliwa tajiri lazima ufe tajiri?. Amka chukua hatua. Zipo nadharia kuwa “Ukipenda pesa ni chanzo cha maovu”? au “Ukiikosa pesa ndo chanzo cha maovu”?. Is the love of money a source of all evils or the lacky of money is a source of all evils?
Kama Kuipenda pesa ni chanzo cha maovu kwanini mara nyingi unahangaikia kutafuta pesa ili kuyakabiri maisha yako? Na kama Kutokuwa na pesa ni chanzo cha maovu, Je umefanya juhudi gani kuondokana na hili tatizo. Sababu kubwa ya tajiri kuendelea kuwa tajiri na masikini kuendelea kuwa masikini, na wenye kipato cha kati wanaendelea kusotea pesa ni elimu kuhusu pesa. Elimu ya kumiliki pesa mara zote inapatikana katika familia tunazolelewa(our domicile), ndo maana utakuta mtu anaweza kuwa Daktari , profesa, au meneja anahangaika na kutafuta pesa kwa sababu elimu aliyosoma ni Taaluma (Proffessional) na siyo elimu kuhusu pesa (lesson of Money). Na hiki ndo chanzo cha wasio na elimu kabisa au elimu ya chini kabisa kuwaajiri walio na elimu kubwa kuanzia digrii moja na hata digrii tatu(PhD). Kumbuka kadri unavyosoma kutoka elimu ya chini kwenda ya juu zaidi ndivyo unavyokuwa mtegemezi wa ajira (employment dependant). Aidha tatizo hili linaweza kuwa katika mfumo wa elimu zitolewazo mashuleni kushindwa kuoanisha na maisha halisi katika jamii mbalimbali. Hii inasabisha walio matariji wanaendelea kuwa matajiri na masikini kuendelea kuwa masikini kwa sababu elimu ya pesa iko katika familia tunazotoka. Ni imani yangu utakuwa unaelewa kuwa maadili yatolewayo katika familia masikini juu ya elimu kuhusu pesa na maadili yatolewayo katika familia tajiri. Umewahi kusikia maneno haya; “Mwenye nacho huongezewa?”. Sina hakika kama unajitambua kuwa wewe ni miongoni mwa wanaopaswa kuwanacho. Familia tajiri nyingi zimeendelea kuongezewa kwa sababu elimu kuhusu pesa wanairithisha kwa watoto wao hivo kujikuta kizazi hadi kizazi wanafurahia matunda ya utajiri. Kumbuka utajiri ni haki yako na hii ni zawadi kutoka kwa Mungu aliyekuumba; Je kwa nini usiichukue zawadi hii?
Familia masikini nyingi sana hazikai kuwaandaa watoto (Child mentoring) kisaikolojia namna ya kuja kumiliki pesa badala yake zinasisitiza namna ya ufaulu… 

Soma Zaidi Kitabu Cha Mshahara ni Chanzo Umasikini