MAPENZI MAZITO YA GRACE NTOMBIZODWA KWA MUGABE NDANI YA IKULU YA ZIMBABWE KABLA NA BAADA YA KIFO CHA AMAI SALLY FRANCESCA HYFON.
Hakika hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe ama kwa lugha nyepesi ni kwamba hakuna binadamu atakayeishi milele katika hii dunia iliyojaa chuki vimbwanga na Visasi lakini mbali na yote hayo binadamu ni wapitaji tuu yaani Duniani tumekuja kutembea.Baada ya First Lady wa kwanza wa Zimbabwe kuugua kwa mda mrefu pamoja na Stress za ndoa yake kuyumba tangu kuumwa kwake Sally Hyfon alifariki Dunia mwaka 1992 baada ya ini lake kushindwa kufanya kazi sawa sawa ambalo lilianza kumsumbua tangu mwaka 1980s mpaka kupelekea kushindwa kubeba Mimba .
Kabla ya kufikwa na mauti katika kitabu cha DINNER WITH MUGABE kinaeleza wazi kwamba kabla ya kuaga Dunua Sally Hyfon alimuuliza Mugabe kwamba najua kwamba una mahusiano na mwanamke mwingine kwa mda mrefu sasa ila naomba uniambie kwamba hata nikifa utaendelea kunipenda na kunikumbuka katika maisha yako yote, maneno machache yenye uzito wa kipekee hayo yalimfanya mtu mzima Robert Gabriel Mugabe abubujikwe ama atoe machozi yaliyokuwa yamejaa hudhuni na uchungu moyoni,hata hivyo Mugabe alimjibu mke wake huyo kipenzi ambaye alitoka naye Ghana kwamba hataacha kumpenda hata pale atakapokuwa ameaga Dunia maneno hayo yalimfanya kutabasamu kiasi kuashiria kwamba anakubali maneno ya mmewe Mugabe kwamba atampenda na kumkumbuka Daima.
Sally aliugua muda mrefu sana na kwenye kitabu cha "Dinner With Mugabe"Inaelezwa kuwa kipindi akiumwa alikuwa najuaa fika kwamba Mugabe ana mwanamke mwingine na alimfahamu vyema Grace kwamba ndiyo alikuwa ana husika na Mugabe alianza mapenzi na binti mdogo wakati huo ni baada ya kuona Sally anaumwa na kulingana na madaktari walinwambia Mugabe wazi kwamba mke wake hataweza kupata mtoto maisha yake yote hivyo kama anataka watoto atafute mwanamke mwingine hata ivoo huo ulikuwa ni Ushauri kutoka kwa madaktari waliokuwa wana mtibu Sally Hyfon. lakini shinikizo kubwa lilitoka kwa mama yake mzazi maarufu kama Bona ambaye alikuwa anamsumbua Mugabe kwamba anahitaji wajukuu hivyo hakukuwa na namna Mugabe angeweza kufanya zaidi kuanzisha uhusiano mpya na Grace ambaye alikuwa anafanya kazi hapo hapo ikulu kama Secretary wake.
Ujio wa Grace Ntombizodwa haukuwa ujio wa kawaida mana kuna mabonde na milima ambayo aliyapitia mwanamke huyo mwenye maono ya kutaka kuibadilisha Zimbabwe katika ulimwengu wa kipekee sana.Mwana mama huyo alizaliwa mnamo tarehe 23/07/1965 nchini Afrika kusini katika mji mdogo kwa wakati huo uliofahamika kama Benon mashariki kidogo mwa jiji la Johnnesburgy akiwa kama mtoto wa nne (4) kati ya watoto watano kutoka kwa Baba yake aliyekuwa anafanya kazi kwenye migodi ya Makuburu nchini humo.kulingana na utulivu kuwa ngumu na hafifu nchni humo kutokana na utawala wa kibaguzi kushamiri sana katika taifa hilo la Madiba alishindwa kuvumilia na mnamo mwaka 1970 alikimbilia nyumbani kwao zimbabwe kuishi na mama yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Idah Marufu uku wakimuacha Baba yao akiendelea kufanya Vibarua nchini humo na kuwatumia matumizi nchini Zimbabwe japo mara chache sana.
Maisha ya Grace Ntombizodwa miaka ya 1970s yalikuwa Magumu mno maana baada ya kuanzi kuishi na mama yake pamoja ndugu zake hali haikuwa nzuri sana kiuchumi mpaka mara nyinge walikuwa wanasaidiwa na majirani kwenye upande wa Chakula na ada ya shule.Alikuwa mda mwingi anaishi na mama yake kwa jina la Mbuya Marufu ambaye ameishi pasipo mme wake kwa mda mrefu sana,Mama yake Grace Ntombizodwa alikuwa anakaa mda mrefu pasipo kunana ama kutumiwa chochote kutoka kwame wake ambaye alikuwa anafanya kazi migodini uko Afrika kusini.Taarifa zinadai kwamba mwana mama Mbuya Marufu alikuwa anatengwa sana na Majirani zake kwa madai kwamba angewaibia mabwana zake maana yeye hakuwa na mme.Maisha ya Grace Ntombizodwa ya utotoni yalikuwa Magumu na yeye kukatisha tamaa maana hawakuwa wanajua hatima ya maisha yao maana kuna wakati walikuwa hawajui ya maisha Baba yao mzazi Kule alikokuwa maana kwa wakati huo hata kupata Barua kulikuwa ni kugumu mno.
Yeye mwenyewe Grace Ntombizodwa akiwa anahutubia 30/08/2018 katika msina wa mama Yake Idah Mbuya Marufu alikiri kwamba mama yake hakuwa mwanamke wa kawaida,alimsifia sana mama yake kwa ni malkia wa Kweli na ni shujaa kwani anastaili sifa na pongezi maana alivumilia shida kwa mda mrefu kipindi wanaishi maisha ya Chini na ya kubangaiza miaka hiyo ya 1970s kabla ya kuolewa na kuanza kuona Mwanga.
Anafafanua kwamba mbali na kwamba Baba yao mda mwingi alikuwa yuko Afrika kusini ila Mama yao huyo alipambana katika kuwalea japo kuna wakati alikuwa akisaidiwa na Majirani,Grace anafafanua yote haya katika msiba wa mama yake kwamba maisha hayakuwa marahisi kwao kwani kuna wakati walichekwa sana kulingana maisha ya chini na ya kimasikini ambayo walikuwa wanaishi lakini hata hivyo Mama yao Idah Mbuya Marufu hakukata tamaa kamwe aliendelea kuwalea katika maadili na kuwatia Moyo kwamna hawapaswi kukata tamaa.Mama yake Grace Ntombizodwa aliagwa Dunia tarehe 30/8/2018 katika msiba huo ambao ulihudhuriwa na familia nzima na Mugabe na Ikulu ya Emmason Mnangagwa.
Katika maisha yake ya utotoni Grace NtombiZodwa alikuwa msichana mpole sana asiyokuwa na Kibri,alikuwa hana makuu yoyote yale alipendwa na kila mtu kwa wakati huo,ila kadri siku zilivyokuwa zunakwenda alianza kubadilika taratibu.Mnamo mwaka 1984 kulingana na Ugumu wa Maisha nyumbani kwao aliamua kuolewa na kamanda Stanley Goreraza ambao alikuwa ni Rubani katika Jeshi la Zimbabwe kwa wakati huo.
Grace Ntombizodwa aliolewa akiwa na Miaka kumi na tisa pekee (19) na mwaka huo huo akiwa katika ndoa alifanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza kwa jina la Russell Stanley Goreraza ila ikumbukwe pia wakati huo huo Mwana mama alikuwa tayari anafanya kama kala ama Typist/Secretary katika Ikulu ya Robert Gabriel Mugabe.Ndoa yao wawili hawa haikuwa na Utulivu kabisa maana tayari ilianza kuyumba miaka ya 1986.Mwana Mama Grace alikuwa tayari amekwisha anzisha mahusiano kwa siri na mtaalamu Robert Mugabe ndani ya Ikulu uku watu wache wakiwa wanajua kinachoendeleq akiwemo dada mkubwa Wa Mugabe na maofisa wachache ndani Ya Chama Cha ZANU-PF.
Wanasema kwamba Viongozi wengi ambao ni madictator wana Utamaduni wa kuwachukua ama kuwaowa wake za watu wengine kinguvujapo sina hakika na Tuhuma hizi,ila ukiangalia kwenye historia ya wababe wengi wa Dunia utagundua kwamba wababe wengi dunia walioa ama kuwachukua wake wa za watu.Grace Ntombizodwa akiwa bado yupo kwenye ndoa yake na mme wake Stanley Goreraza alianza mahusiano na Mugabe Ikulu,mpama kwenye msiba wa Mama mkwe wake tarehe 30/08/2018 Mugabe alidai siku moja Ikulu alimwambia Grace kwamba "Nakupenda" lakini Grace hakujibu swali hilo lakini alipomfuata na kumkubatia Grace alikubali kukumbatiwa na hata Mugabe alipo mkisi Grace hakusita bali alipokea Busu.
Kulingana na tendo hilo la Mugabe kumbusu basi Kimoyo moyo Mugabe aliamini kwamba Grace anampenda na hapo ndipo mahusiano yalipoanzia lakini wakati huo Sally Hyfon anaumwa Vibaya mno (Battling Sick).iwe tu akilini kwamba wakati huo wote walikuwa kwenye ndoa na ndo hapo walipoanza kuchepuka ndani ya Ikulu kwa siri kubwa uku Grace akijua fika kwamba Sally Hyfon uko hai na anaumwa vibaya mno,Grace alibadirika katika Umri wa miaka 30s na kuwa mwanamke aliyetaka Utajiri mkubwa cheo kikubwa na njia pekee ilikuwa kuolewa na Robert Gabriel Mugabe.
Sababu kubwa iliyopekea Mugabe Kuanzisha Mahusiano Ikulu na Grace Mugabe iilikuwa ni nini haswa..??Mwaka 2013 akiwa kwenye Interview na Dali Mpofu alidai kwamba alikuwa anataka kumzalia Mama yake Bona Mjukuu maana Mke wake Sally Hakuwa ana uwezo tena wa kumzalia mtoto kulingana na Utabibu wa madakari.Lakini pia jambo hili liliwekwa wazi katika maarufu Cha Haidi Holland kinachojulikana kama DINNER WITH MUGABE kilichotoka mwaka 2008 kimeelezea kinaga Ubaga kwamba Mugabe alipata Shinikizo kubwa kutoka kwa mama yake mzazi anayefahamika kwa Jina la Bona kwana alikuwa anataka mjukuu kabla hajafa.
Hivyo Mugabe aliheshimu mawazo ya mama yake na hakuwa na namna maana tayari kulikuwa na mwanamke mzuri mno ndani ya Ikulu hivyo llibidi kuanzisha mahusiano lengo kuu likiwa kumpata ili kumfurahisha mama yake mzazi kwa Jina la Bona na ndipo penzi liliponoga katika ya Grace na Robert Mugabe na mpaka kufikia hatua kupata mtoto wa kwanza nje ya ndoa mwaka 1988 hapa bado Grace Ntombizodwa Akiwa bado yupo na mme wake Stanley Goreraza na mtoto huyo alipewa jina la Mama yake Mugabe yaani Bona na huyu akiwa mtoto wa pili wa Grace Ntombizodwa uku akiwa wa kwanza kwa Mugabe.
Grace Mugabe alianza mahusiano na Mugabe akiwa katika Umri wa Miaka 20s na mda wote ambao Grace anajihusisha na Mahusiano ya kimapenzi First Lady Sally Hyfon alikuwa anajua kila kitu japo Kugabe alikuwa anafanya siri lakini mke wake alikuwa anajua fika yote hayo yanayoendelea na Sababu kubwa ilikuwa ni kwa Sally Kupoteza Uwezo wa kuzaa.Pengine Sally angekuwa ana uwezo wa kuzaa leo tungekuwa tunazungumza Mengine juu ya Mugabe na Grace.
Wanasema kwake tutarejea lazima mnamo tarehe 27/01/1992 Sally Hyfon kulingana na Ugonjwa wa mda mrefu ulikuwa unamsumbua Sally aliaga Dunia na kuliacha Taifa likiwa katika simanzi nzito juu ya kuondokewa na mama ya mpendwa ambao wana zimbabwe walipenda kumwita AMAI yaani maana yake Mama ni jina lenye heshima kubwa mno nchini humo.Wanazimbabwe walimpenda sana mwana mama Sally aliyeamua kutoka nyumbani kwao Ghana na kuhamia Zimbabwe tayari kuongozana na Mugabe katika kulijenga Taifa waswahili wanasema kwamba kizuri hakidumu kamwe na huo ndio ulikuwa mwisho wa Sally Francesca Hyfon.
Siku wanasema hazigandi daima,mambo mengine yanafanyika katika maisha yetu siyo kwa sababu tulipanga kuyafanya ama kututokea hapana ila kuna mazingira fulani na changamoto tunazokutana nazo katika maisha yetu ya kila siku ndio yanatufanya tubadilike tabia pamoja na mtazamo.Mwaka 1992 akiwa bado kwenye ndoa yake ya kwanza alikuwa tayari amepata mtoto wa pili kwa Mugabe aliyepewa jina la Baba yake Robert Peter Mugabe Jr huyu anakuwa anakuwa pili kwa dada yake anayefahamika kwa jina la Bona ambaye nimemuelezea hapo juu.
Grace Mugabe hakuishia hapo Mwaka 1994/1995 aliamua kuvunja ndoa yake mwenyewe kwa kuomba taraka kwa mme wake Stanely Goreraza pasipo sabu za msingi ila aliamua mwenyewe baada ya penzi kukolea ndani ya Ikulu ya Robert Gabriel Mugabe.Hata ivo mwanamke akiamua kuondoka wanasema huwezi kumrudisha kamwe Kamanda na Rubani aliamua kumpa taraka kinyonge sana maana alijua fika anachukuliwa na boss wake wa kazi.
Mwaka 1996 Grace Ntombizodwa aliamua Kufunga harusi ambayo wenyewe waliiita (Wedding of The Century) yaani Harusi ya Karne ilikuwa ni harusi kubwa na ya gharama kubwa nchini humo na tayari Grace Ntombizodwa akaweka historia nyingine ya aina yake nchini Zimbabwe yaani akawa First Lady wa pili Tangu Uhuru wa Taifa hilo mwaka 1980 na kwa upande wa Mugabe ikawa ndiyo harusi yake ya pili katika Maisha yake ya kwanza ilikuwa mwaka 1961 aliyofunga na Amai Sally Hayfon.
Wakati ndoa hiyo inafungwa Mwana mama Grace alikuwa ana Umri wa miaka 31 uku Mzee Mugabe akiwa na Umri wa Miaka 72,Baada ya ndoa hiyo kufungwa mwaka 1997 Walifanikiwa kupata mtoto wao wa tatu aliyepewa jina la Chatunga Berlmine Mugabe ambaye kwa sasa ana miaka 21,watoto hawa wanaishi maisha ya kifahari sana uko Afrika kusini na kutembelea Gari zenye Gharama kubwa ambazo zinafanana na wachezaji wa mpira Barani Ulaya ni moja ya Vijana Maarufu sana Afrika kusini na Afrika kwa Ujumla wake na wanapendwa kuliko kawaida na mama yao Grace Ntombizodwa Mugabe.
Grace Ntombizodwa Mugabe ni mwana mama mwenye malengo makubwa na anayeamini kwamba kila kitu kinawezekana ni suala la mda tu na malengo (Aspiration),Grace ni moja ya wanawake wachache waliopata umaarufu mkubwa Duniani kulingana na maisha aliyoyachagua kuishi.Grace Ntombizodwa Mugabe ni moja ya wanawake waliojaribu kutingisha na kuleta mageuzi makubwa katika Siasa za Zimbabwe katika pande zote mbili kuharibu na Kujenga pia anapenda makubwa yaani Cheo lakini pia anapenda kuongoza yaani ana kipaji cha Uongozi na anaamini anaweza kuongoza Nchi pasipo kuyumbishwa hakubali kushindwa kizembe ni mpambana aliyejidhatiti na ni mtafutaji haswa siyo mwanamke aliyekaa tu ndani hapana bali ni mbunifu na anajituma mbali na kwamba ana maadui wengi ndani na nje ya nchi na hii inatokana na Harakati zake kisiasa.Ni mwanamke ambaye ambaye kwa namna moja ama nyingine siyo mtu ambaye anaweza akavumilia jambo lolote lile litakalo pita mbele yake.