MAPUNGUFU YA KITAALUMA KATIKA KONGAMANO LA CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA (TLS).
January 12 2019
Tanganyika Law Society ni chama cha Wanasheria kwa upande wa Tanganyika tu,(Bara) Chama hiki kilianzishwa kwa Sheria ya Baraza la Kutunga Sheria (Legislative Council) Namba 30 ya 1954 na ni moja ya Sheria nyingi za iliyokuwa Tanganyika kabla ya Uhuru, ambazo kwa mujibu wa Kifungu cha 4 cha Katiba ya Tanganyika ziliruhusiwa kuendelea kutumika Tanganyika ilipopata Uhuru Disemba 9 mwaka 1961 kama Sheria za Tanganyika huru.
Mamlaka ya Baraza la Uongozi la TLS katika Kutekeleza Majukumu ya Umma ni kusaidia kuboresha elimu ya sheria na taaluma ya Sheria Tanzania na kuwawezesha wanataaluma wa sheria kupata elimu ya ziada ya sheria kwa kadri mabadiliko yanayotokea nchini na duniani.
TLS ni Taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria za nchi kabla ya Uhuru na kukubalika kuendelea kuwepo kama Taasisi ya Kisheria kwa malengo ya kuanzishwa kwake kuelekezwa kwenye manufaa ya umma kwa kushirikiana na Mahakama, Bunge, pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
KUCHUKUA MAONI YA WANASIASA.
Kama kuna jambo Tanganyika Law Society ni chama cha Wanasheria TLS wamekosea ni pamoja na kwenye eneo hli la kuchukua na kukusanya maoni ya wanasiasa kuhusu Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya vyama vya siasa Nchini,
Wanasiasa waliokusanywa kwenye KONGAMANO la Chama cha wanasheria Tanganyika TLS kupitia vyama vyao na Asasi zingine mbalimbali wanayo fursa ya kutoa maon yao kwenye Kamati ya Bunge kwa mujibu wa Sheria, Utaratibu na Kanuni za Bunge,
Hivyo kuchukua maoni ya wanasiasa wa mlengo mmoja (WAPINZANI) ndio kuwasaidi au kutumia Taaluma yao ya kisheria kwa manufaa ya Watanzaia? Na dhani hii sio sahihi kwanza wanasiasa hawa kupita vyama vyao wanayo nafasi ya kujadili Muswada kwenye vikao ndani ya vyama vyao na kupeleka maoni yao kwenye Kamati ya Bunge, Lakini pia Tanganyika Law Society ni chama cha Wanasheria TLS kama wataalamu wa Sheria kupitia Baraza lao la Wataalamu wailpaswa kukutana kuchambua Kitaalamu na Kupeleka maoni yao mbele ya Kamati kama TLS.
Kushindwa kufanya hivyo ni kushindwa kwa TLS kutekeleza majukumu yake ya Kitaluma na badala yake kufanya shughuli za Kisiasa,
Kama Wanataaluma wa Sheria walipaswa kukaa kwenye Baraza lao na kuchambua Muswada Kifungu kwa Kifungu na kuandaa Maoni ya Taasisi yao, Kufanya kinyume na hivyo TLS wamewadhulumu watanzania haki ya kufaidika na Watalamu hawa wa Kisheria waloamua kujiingiza kwenye shughuli za kiharakati na kisiasa kwa nembo ya TLS.
NINI MAANA YAKE?
Kwa kutumia Utaratibu huu wa TLS huwezi kuona tofauti yoyote ya kimsingi kati ya maoni ya Wanasiasa (UPINZANI ) na maoni ya watalamu wa Sheria (Tanganyika Law Society TLS) mbele ya Kamati ya Bunge.
Hili ndilo kosa la kuchagua Viongozi wa kisiasa kuongoza vyama vya Kitaaluma, Tanganyika Law Society TLS sasa ni chama cha kisiasa kisicho na Usajli wa muda wala wa Kudumu, Hakuna tofauti kubwa kati ya KONGAMANO la Zanzibar likiongozwa na Maalim Self na Kongamano la TLS D'Salaam likiongozwa na Rais wa TLS Bi Fatma Karume Maaufu kama SHANGAZI, hata washiriki ni wale wale na Malengo ni yale yale.
Kibaya zaidi wasomi wetu hawa wa Kisheria wanafanya kazi ya kukusanya maoni kinyume kabisa na Utaratibu, Shughuli ya kukusanya au kupokea maoni ya wadau ni shughuli ya Kamati ya Bunge sio chombo chochote kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Bunge,
.
TLS WANAIMBA WIMBO ULE ULE.
Badala ya kukaa kwenye vikao vyao kama chama cha wanasheria Tanganyika kujadiliana Kifungu kwa Kifungu na kubainisha mapungufu sambamba na kupendekeza mabadiliko ili kuboresha Muswada, TLS nao wanaungana na wanasiasa wa UPINZANI kulalamika uwepo wa Muswada kwa hoja za kipuuzi.
Wanasiasa (WAPINZANI) wanalalamika uwepo wa kifungu cha Kinga kwa Msajli wa vyama wakati akitekeleza majukumu yake, na TLS wanalalamika hivyo hivyo, Kama TLS wangekwenda mbali zaidi kwa kujisomea Muswada na wakasoma Sheria iliyopo sasa wangegundua kwamba jambo la kinga kwa Msajili sio Jipya lipo kwenye sheria Na 5 ya mwaka 1992 Sura Namba 258 kifungu cha (6).
Lakini kwa sababu TLS sasa wameamua kuendesha chama cha wanasheria Tanganyika kwa hisia (MIHEMKO) ya kisiasa, hivyo wanakosa muda wa kupitia Sheria liyopo ya vyama vya siasa na Muswada kifungu kwa kifungu.
Makosa yanayofanywa na wanasiasa (WAPINZANI) kwenye kuchambua Muswada kutokana na Uchache wao wa Maarifa na waledi wa Kisheria hayakupaswa kufanywa na Chama cha wanasheria Tanganyika TLS, Wakati wanasiasa hawataki kusoma Muswada sambamba na Sheria iliyopo na TLS nao wanafanya hivyo hivyo UNLESS OTHERWISE kuwapo na mkakati maalumu wa kuliendea suala hili KIPROPAGANDA.
Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa Mhe John Shibuda anayo nafasi ya kushauriana na Msajili wa vyama lakni hakutaka kutumia nafasi hiyo na pia kupitia Baraza lake kama Kiongozi mkuu angeweza kuandaa maoni ya Baraza la vyama vya siasa na kupeleka kwenye Kamati ya Bunge, sio kuja kushutumu Muswada kwenye KONGAMANO la Chama cha wanasheria TLS ambao na wao watapeleka maoni yao kwenye Kamati ya Bunge.
Ni masikitiko makubwa sana Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa Mhe John Shibuda amejikuta anatoa HISTORIA kwenye Mchango wake Katika KONGAMANO hilo la Chama cha wanasheria TLS, Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa Inaonyesha hajasoma Muswada wala Sheria iliyopo, Kabla ya kutoka na kueleza chochote alipaswa kupitia ili badala ya kueleza HISTORIA angejikita kwenye Vifungu katika Muswada na maoni yake kwenye maeneo anayohisi ni tatizo kwa Upande wake.
Sina hakiika kama kulikuwa na mashindano ya kumtafuata anayejua HISTORIA ya mfumo wa vyama vingi au maelezo yake yametoa msaada gani kwenye uchambuzi wa Vifungu vya kishera?
Mwenyekiti wa Baraza alipaswa kuonyesha SERIOUSNESS ya kuchambua Vifungu vya Muswada na Sheria iliyopo na sio kuonyesha uhodari wa kumiliki MISAMIATI ya kutosha.
Kwa sura hii, hakuna Ubishi wowote kwamba kuna pesa nyingi sana zimetolewa kutoka nje kwajili ya kukwamisha Muswada huu, Kama TLS na Baraza la vyama wote hawa wana haki sawa (FURSA) ya kutoa maoni yao kwenye kamati ya Bunge, wamepatwa na nini mpaka wanakwepa Utaratibu wa Kisheria na Kikanuni?.
TLS NA WAPINZANI WAGEUKA WAPIGA RAMLI.
Tanganyika Law Society ni chama cha Wanasheria Tanganyika TLS na Wapinzani wamejiunga kwenye ''DHAMBI YA KUDHANI'' huu ni Utaratibu mpya kwa Nchi yetu, WAPINZANI wanasema Kama Mchakato wa Muswada ukiendelea Bungeni unaweza kuongezwa mambo mengine mabaya zaidi kuliko yaliyopo sana na huu ndio msimamo wa Tanganyika Law Society chama cha WanasheriaTLS.
Kwanza suala la kuwapo (SCHEDULE OF AMENDMENTS) ni Utaratibu halali wa Kisheria kwa mujibu wa Kanuni za Bunge letu na wabunge wote wakiwemo na Wabunge wa UPINZANIA wamekuwa wakitumia fursa hii muhimu warekebisha Miswada mbalimbali ya Serikali,
Hoja kwamba kutakuwapo na Shedule of Amendment za wabunge wa CCM hivyo Muswada uondolewa n hoja ya KIPROPAGANDA baada ya kushindwa kujenga hoja ya kukosoa Muswada,Watanzania wamekwisha tambua knachopiganiwa na maslahi ya viongozi wa vyama kutaka kumliki vyama kama SACCOS na kutafuna pesa za RUZUKU ya vyama.
Kwa Utaratibu wa Nchi yetu hatujawahi kushughulika au kushiriki kwenye ''DHAMBI YA KUDHANI'' Muswada upo wazi tujielekeze kutoa maoni yetu kwenye Muswada ili tupate Sheria Bora kwa Afya ya Demokrasia ya Nchi yetu,
TLS NA WAPINZANI WAKWEPA VIKAO.
Kama ilivyo kwa vyama vya UPINZANI hawana muda kuitisha vikao vyao halali vya Kikatiba kujadli Muswada badala yake wale wajanja wachache wanaendelea kumiliki mawazo ya vyama na TLS nao wamefanya hivyo hivyo,
Baraza la Uongozi la TLS katika Kutekeleza Majukumu yake walipaswa kuitisha kikao cha Baraza kujadili Muswada Kifungu kwa Kifungu na kuandaa maoni ya TLS kisha kuyapeleka kwenye Kamati ya Bunge,
Lakini Viongozi wa TLS na WAPINZANI hawana muda wa Vikao kila kitu wanamaliza viongozi hata kwa mambo muhimu kama hili la Muswada. Utamkuta Doyo Hasan Doyo Shibuda, Zitto Kabwe Mnyika Dovutwa,na Rungwe POVU lkiwatoka kuhusu Muswada lakini hawajawadi kuitisha Kikao chochote cha Chama kujadli Muswada na kupeleka maon yao kwenye Kamati ya Bunge.
Huu Muswada ndio unakwenda kuondoa MADUDU kama haya ya kugeuza vyama kuwa ni SACCOS za wajanja wajanja na kuvifanya vyama sasa kuwa TAASISI za Umma kwajili ya wanachama wote wa chama husika.
TLS NA WAPINZANI WANALILIA PESA TU,
Kalele zote hizi za WAPINZANI na TLS ni kutokana na kifungu cha Kisheria kwenye Muswada pendekezwa kitakachompa mamlaka Msajili wa vyama vya siasa kuhoji matumzi ya RUZUKU ya vyama vya siasa. Lakini pia kuhoji au kupata taarifa ya pesa zote za vyama zinazoingia Nchni kwa kigezo cha mafunzo na aina ya mafunzo hayo,
TLS na WAPINZANI hawataki Ruzuku za vyama kuhojiwa ili watanzania waendeleo kuona MADUDU kama yale ya RIPOTI ya CAG liyoonyesha kiasi cha Biloni mbili Pesa za Kitanzania M/kiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alimkopesha shemeji yake Ruzuku ya Chama Au waone UTUMBO kupitia Ripoti hiyo hiyo ya CAG inaonyesha Chama ACT- Wazalendo kinachopata Miloni nne na laki tano kwa mwezi lakini kina HATI CHAFU,Au waone Maalm Self anachota RUZUKU ya CUF Kiasi cha Milion 800 na kumkopesha Juma DUNI na kiasi cha Milion 100 anamkopesha Juma Nkumbi.
Kama Zitto Kabwe na chama chake cha ACT-Wazalendo wanashindwa kusimamia RUZUKU ya Milioni nne na laki tano unategemea nini kwa watu hawa ukiwapa HAZINA ya kusimamia pesa za Nchi kubwa kama Tanzania? Halimashauri zote zinazosimamiwa na CHADEMA na ACT Wazalendo zimetajwa kuwa na HATI CHAFU.
Watu kama hawa huwezi kushangaa Ukiwaona wanapinga kuwapo kwa kifungu cha kudhibiti Matumizi ya RUZUKU ya vyama vya siasa.
HITIMISHO
Kwa mujibu wa madhumuni ya kutaka mambo yanayogusa Maslahi mapana ya Watanzania yapate jukwaa lenye Utanzania, basi chama hiki (TLS) kingekuwa makini zaidi na kuunganisha malengo na matarajio katika utaifa huo, na kuongoza mijadala na makongamano husika kwa kuzingatia Sheria na taratibu TLS hawakupaswa kukusanya maoni kwa wanasiasa . Ila kama TLS kinataka kutoa waende kwenye kamati ya Bunge