Monday, January 14, 2019

NG'WANAMALUNDI (MWANA MALUNDI), MTU WA MAAJABU



Yawezekana umewahi kusoma au kusikia historia za makabila mbalimabli, hasa ya Wasukuma na Wanyamwezi, lakini huenda hukupata kusikia habari ya Ng’wanamalundi kwa undani zaidi. Wapo wengi wamejaribu kumsimulia lakini si kwa undani zaidi.
Kwa wakristo, ukisoma habari za Yesu utaona maajabu aliyofanya yakiwemo ya kutembea juu ya maji, kuzuia dhoruba ya mawimvi ya bahari na yakamtii, n.k Ng’wanamalundi nae amefanya maajabu yanayofanana na hayo likiwemo ya kutenganisha bahari kukawa na barabara na kupita akitembea kama nchi kavu, kulima viazi asubuhi na jioni akaenda kuvuna, kukausha miti n.k. Kwa Undani zaidi soma habari zake katika kitabu hiki.

Utangulizi

Ng’wanamalundi alizaliwa katika ukoo wa kawaida kijijini Mwakubunga Nera wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza. Makuzi yake yalikuwa chini ya wazazi wake mzee Bugomola na Ngolo Igulu hapo kijijini. Ng’wanamalundi anaitwa mtoto wa dawa kwa sababu baba na mama yake huko nyuma uzazi ulikuwa wa shida shida hivo kupata mtoto ilifika mahala ikawa ni tatizo kubwa. Mara baada ya baba yake kuhangaika sana mwisho aliamua aende kwa Mganga wa jadi. Alipofika kwa mganga huyu, mzee Bugomola alipewa maelezo ya masharti na Mganga wa Jadi kuwa akubali kufa mara baada ya mtoto kuzaliwa. Mganga wa jadi ali mueleza mzee Bugomola kuwa atapewa dawa ataitumia na watapata mtoto wa kiume mwenye maajabu sana. Hivyo mzee Bugomola alikubaliana na masharti ya maganga wa jadi na akapewa dawa akatumie. Inaelezwa kuwa mzee Bugomola amefariki mara baada ya Mtoto kuzaliwa na mtoto alipewa jina la Igulu.
Alipokua na kufikia makamo alianza kucheza ngoma. Alipofikia umri wa miaka ishirini aliondoka nyumbani pamoja na vijana wenzake wawili wa pale kijijini kwenda kwa bibi kizee aliyekuwa maarufu sana ili kupata dawa ya 'Nsamba'. Nsamba ni dawa ya kisukuma (Nitailezea baadae). Dawa hii ilimfanya awe mcheza ngoma mashuhuri sana. Hata   hivo maandiko…….

Zaidi Soma kitabu

               Email: masele97@yahoo.com 
Simu: 0783-846901