Monday, January 14, 2019

Je Wajua maana ya Neno "Wasukuma"?

Je Wajua maana ya Neno "Wasukuma"?

Kabila la wasukuma ni changa kuliko makabila yote ya Tanzania bara maana historia ya kabila hili haiendi nyuma zaidi ya mwaka 1500 ambapo miaka hiyo makabila mengi ya Tanzania yalikuwa yanatambulika.
Katika Kitabu cha jumuiya ya watemi wa kisukuma kiliandiaka kuwa miaka ya 1550, kabila la wasukuma ndio lilianza kujikusanya na kutengeneza makao maalumu. Utafiti unaonesha kuwa kihistolia kabila hili halikutoka nje ya Tanzania (primary immagrant) kama ilivyo kwa makabila mengine. Kabila hili lilitokana na mwingiliano wa kuoana (intermarriage) baina ya makabila yaliyokuwa yakitokea nje na kuingia Tanzania yakiambaa mashariki na magharibi mwa ziwa victoria. Mpaka katikati mwa karne ya 14, iliingia misafara ya wahamiaji wengi kutoka Uganda, Kenya, Sudani, Rwanda, na Congo, wakatua kuzunguka ziwa victoria kuendesha shuguli za uwindaji na uvuvi. Wakaanza kuoana na kuanzisha lugha tofauti kulingana na mazingira. Mfano Misafara iliyotoka Kenya, Sudani na Ethiopia ilitua kaskazini mashariki mwa ziwa victoria, mchanganyiko wa misafara hii, ilitengeneza lugha ya Wazanaki, Washashi, Wajita, Wakulya. Misafara kutoka Uganda, Rwanda, Burundi na Congo walitua mgharibi mwa ziwa victoria huku wakizalisha makabila ya Balongo (bakamba au wafua vyuma), Bashi (wawindaji), Bashoma, Bazinza, Washubi. Miaka ya 1400 Makabila ya Magharibi mwa ziwa (yaani Balongo, Bashoma, Bazinza, Bashi, na Washubi) walianzisha biashara ya vyuma vya kilimo na uwindaji wakaanza kuwauzia watu wa Mashariki na kusini mwa Ziwa (Wanyamwezi, Wajita, Washasi, Wazanaki Na Wakulya) biashara hii iliwafanya waanze kuoana na kuzaliana. Mwingiliano (intermarriage) baina ya makabila haya yenye lugha na tamaduni tafauti, baada ya miaka mingi kuliibua Lugha mpya tofuati ikiwa na mchanganyiko wa misamiati na rahaja mbalimbali kutoka lugha mama (Vernacular Language).
Lugha hii ilikua kwa kasi sana kwani hawa watu walikuwa na uwezo wa kuzaliana sana kuliko saidiwa na wingi wa vyakula, samaki na wanyama pori. Mwishoni mwa karne ya 15 watu wa lugha hii ngeni walianza kujikusanya makundi makundi na kuanzisha makazi ya kudumu maeneo mbali mabli kuzunguka ziwa victoria na mapori ya kaskazini mashariki mwa Tanzania. Kabila hili badae lilitambulikana kwa majina tofauti tofauti kulingana na mahali. Mfano Wajita waliwaita WAGWE na Washashi waliwaita WAKLITI. Mnamo mwaka 1550 watu hawa walianza kuambaa kusini (dakama kwa kisukuma) ambapo..... 

Soma Kitabu cha Historia ya Wasukuna Na Ng'wanamalundi kwa undani Zaidi.