Elimu Kuhusu Pesa
Usichokijua
kuhusu pesa
Ndicho chanzo
cha tatizo
la pesa
maishani mwako.
Unawareness
of money lesson is the source of money problem in your life.
|
Ipo haja kubwa kwa watu kuelimishwa umuhimu wa kujitegemea kiuchumi.
Watu wengi hupata elimu kutoka shule au vyuo mbali mbali kila mmoja kutokana na
matakwa ya taaluma anayohitaji. Wengine huchaguliwa taaluma fulani na wazazi au
walezi wao na wengine kwa kujikuta anaingia katika taaluma ambayo hakutarajia
kutokana na mazingira Fulani (mfano: Asilimia
kubwa ya waalimu mashuleni nchini Tanzania haikuwa kwa matakwa yao kuanzia
miaka ya 1995). Sina tatizo na kuwachagulia taaluma ambayo aidha mzazi au mlezi
angependa mwanae asomee au kuingia katika taaluma ambayo haikuwa ndoto yako
toka awali. Swali la msingi hapa “Taaluma
uliyochagua au kuchaguliwa au kuingia pasipo matarajio imekuandaa kujitegemea
kiuchumi kikamilifu?” .
Kitabu cha Mshahara ni Chanzo ch Umasikini Kimeeleza kiundani zaidi