LEON TROTSKY NA VLADMIR ILANOVA LENIN KATIKA UTAWALA WA URUSI
VLadmir Ilanova Lenin kama mwasisi wa taifa la kijamaa Urusi basi tambua hakuwa peke yake ,maana haikuwa kazi rahisi kabisa.siku zote huwezi kufanya kitu mwenyewe lazima utaitaji msaada fulani kutoka kwa ndugu zako au marafiki zako,hivyo mwaka 1917,kipindi yanafanyika mapinduzi makubwa ya kumuondoaa mfalme Nicholas II na mke wake Alexandria Victoria Hellena,alikuwepo mtu mmoja anaitwa Leon Trotsky,huyu ndiyo alitoa mchango mkubwa katika kufanikisha kuingiza utawala mpya wa bwana Vladmir Ilanov Lenin madarakani kwa wakati huo.
Kifo cha Comrade na mtaalamu wa vita chakavu mzee wa mizoga mibichi uko Urusi comred Leon Trotsky kilikuwa kimepangwa.Mwanaharakati na mwanamapinduzi huyu ambaye alitadhamiwa kuchukua nafasi swahiba wake Vladmir Lenin.Huyo ndiyo alipewa jukumu la kukisuka kikosi cha jeshi la Urusi na kuja kuunda kikosi kinaitwa REDARMY kilichomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kutoka mwaka 1917 mpaka 1922 na hapo ndipo alipata heshima kubwa kutoka Vladmir Lenin na watu wa Urusi.
Huyu bwana kumbuka jina la LEON TROTSKY siyo jina lake alilopewa na wazazi wake,ni jina ambalo alijipa mwenyewe baada ya kutoroka jela,Sasa kuepuka kujulikana akaona ni vyema akabadilisha jina.Ni mmoja ya watu saba wa mwanzo wanzilishi wa chama cha kijamaa Socialist party (workers party),chama cha wa wafanyakazi na rafiki wa karibu sana wa Lenin.Ni kiongozi wa jeshi maarufu kwa jina la REDARMY lililomuweka mtaalamu Lenin madarakani mwaka 1917.
Kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ilitokewa kupendwa mno na mkuu wake Lenin, na mpaka kumpa madaraka makubwa na vyeo vya kutoshaa Serikalin,lakini ikumbukwe tu kwambaa Bwana Leo hakuwa amezaliwa Urusi au hakuwa mrusi,ni mtu mwenye asili ya Israel.Nitakufafanulia kadri tunapotiririka juu ya utata wa kifo chake ,baada ya kuonyesha ujasiri na kuonekana ni mtu ambaye ana malengo mapana na hamu ya kutamani kuona siku moja nusu ya dunia inaamini katika ujamaa, aliamini kabisa siku moja urusi itakuwa Taifa kubwa Duniani ,hivyo alijitoa sana pale alipopataa nafasi ya kufanya hivyo.alikuwa na mapenzi na Urusi na siyo vinginevyo mpaka kupelekea kuaminiwa na chama cha socialist party (bolshevik party).
Baada ya kufanyika mapinduzi mwaka 1917,bado kazi ilikuwa Kubwa zaidi,maana vikosi vitiifu vya Serikali ya mfalme NICHOLAS vilikuwa vinaleta mushikeli na baadhi ya maeneo kulikuwa na upinzani mkubwa sana .Hivyo mwaka 1918 Leon trotsky alipewa jukumu la kuunda kikosi maalumu cha kupambana na vikosi vitiifu vya Serikali iliyokuwepo madarakani kwa wakati huo ,haikuwa kazi rahisi kabisa kwa kuwa Leon, alikuwa mtu makini na aliaminiwa sana na Lenini.Conmred Leon Trotsky akaamua kuunda kikosi ambacho kilikuwa siyo cha kawaida, na vita viliendelea na watu wengi walipoteza maisha na vitu vingi ikiwemo miundo mbinu na mambo mengine kuharibiwa vibaya .
Kikosi hicho kilikuwa na kazi ya kufagia fagia na kuangamiza maadui wote pasipo huruma yoyote ile,Maelfu kwa maelfu walipoteza maisha na kuzikwa katika makaburi ya pamoja, jeshi hilo lilipewa jina la REDARMY.Kikosi hicho kiliundwa na mtaalamu Leon, alipewa amri na VLADMIR LENIN ,kikosi hicho kilimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kutoka mwaka 1918 mpaka 1922 vita hvyo vilivyokoma na baadae kuanza kuunda Serikali mpya chini ya utawala mpya wa bwana Vladmir Lenin, uku Leo akipata jina kubwa na umaarufu mkubwa katika chama chake cha BOLSHEVIK PARTY na dunia kwa ujumla wake .
Leon alifanya mambo mazito katika taifa ambalo siyo lake ,wala hakuwa mzawa wa Urusi ,hapaa inatukumbusha kwamba kuwa mzalendo siyo lazima upiganie nchi yako ,alipenda falisafa za mtaalamu Lenin na waasisi wa mfumo wa communism na kuamua kwenda kumuunga mkono. Bwana Lenini aliyekutana naye uko London baada ya kutoroka jera mwaka 1902, na hapo ndipo urafik wao ulipoanza na baadae kuelekea uko Urusi katika harakati chungu za kuondoa utawala wa zamani wa Mfalme Nicholas, ambaye alikuwa anaongoza nchi kwa kufuata matakwa ya mke wake Alexandria Helena Victoria Melanovina.
Kwa wakati huo,Maisha yaliendelea na mapambano yaliendelea pia,mpaka walipokamilisha harakati zao na kuanzisha taifa jipya la kwanza la kisocialist rasmi mwaka 1924 Nomember.Leo trotsky alijitoa sana mpaka kufikia hatua ya kuingia vitan kwa kupigania uhuru wa taifa ambalo halikuwa lake kabisa.Leon namfananisha na John Okello ambaye alipigania na kufanikisha mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964, baadae kufukuzwa katika taifa hilo kama mbwa mwizi ,hakuna mpaka leo aliyetambua mchango wa wake,hata kuwakumbuka ndugu wa john okello, imekuwa ngumu sanaa ,kuna mmoja kutokea visiwa vya Trinidad Dr Gearge Padmore, ambaye alihusika pakubwa katika kuanzisha umoja wa Afrika (OAU) kwa sasa AU nani anamkumbuka leo ?.
Baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1922,walibakiwa na kazi kubwa na ngumu ya kujenga taifa, baada ya vita kuvuruga vuruga na kuleta uharibifu mkubwa na ndo kipindi hicho mtaalamu LENIN aliutambua mchango mkubwa wa Leon trotsky na kumpa vyeo vikubwa kwenye chama cha Communist Party/Bolshevik party na serikalini.Alipewa nafasi kubwa ya kuwa Waziri wa mambo ya nje wa Urusi.Lakini pia yeye na Lenin walilenga kusambaza Socialism (ujamaa) duniani kote ,waliona mbali kwamba kazi waliobakiwa nayo ni kusambaza falsafa ya ujamaa Duniani kote, hiyo ilikuwa kazi kubwa iliyofanywa na watu hawa wawili.
Walifanikiwa kuishawishi Dunia na vijana wengi kuingia uko kama wakina Fider Castro Ruz uko Cuba Pamoja na Ernest Che Guevara.wakaibuka wakina PADMORE GEORGE ,wakaja vijana wabishi baadae wakina wakina Osagyevo Nkwame Nkuruma na wengine wengi ambao sijawataja akiwemo THOMAS ISIDORE SANKARA.Baada ya miaka Kwenda wakaibuka wakini Julias Kambarage Nyerere ,wote hao walikuwa wafuasi wakubwa wa Falsafa ya kijama.haya yalikuwa mawazo ya Lenini na Leon trotsky ,katika harakati zao za kusambaza falsafa hiyo adimu, hawakutaka kabisa kuishia Urusi pekee walitaka na mataifa mengine yaige huo mfumo uliokuwa unapingwa vikali na Marekani pamoja na wafuasi wake .
Miaka inasonga na vitu vinatokea na kupotea watu wanatokea na kupotea pia,hata kabla VLADMIR LENIN na rafiki yake wa karibu LEON TROTSKY ambaye maisha yake yote amekuwa ni mtu wa kufungwa na kutoroka toroka, mara kwenda Ufaransa ,London ,Urusi Ukrain na baadae kukimbilia mexico.Watu hawa hawakupata kufurahia matunda ya kazi yao kabisa.Walipata kufanya kazi kubwa lakini hawakuonja mafanikio yao ,taratibu mambo yalianza kuvurugika pale Lenin alipofariki gafra mwaka 1924 ,Baada ya mtaalamu Lenin kufa watu wengi walitegemea Leon Trotsky angekuwa ndo mtu pekee ambaye angechukua nafasi hiyo na ndo ilitakiwa iwe ivo.
Lakini hilo halikutokea maana Leon Tronky alikuwa anapanga uku Joseph Stalini na yeye alikuwa anapanga vile vile ,Joseph stalin alikuwa ndiyo katibu mkuu wa wa chama cha Bolshevik Party kwa mda mrefu ,hivyo hakuwa tayari kuona nafasi ile inachukuliwa na mtu baki na yeye akose kabisa ,Stalin alikuwa tayari kuchoma mtu kisu au kufanya chochote ili mradi tu nafasi hiyo aipate,ulitokea mgogoro mkubwa ndani ya chama ambao ulipewa Jina la STROIKA au PARASTROIKA MOVEMENT (Internal Conflicts within Bolshevic Part) au wazungu wanasema STRUGGLE FOR THE POWER.Mpambano ulikuwa mkali ndani ya chama kwamba nani atakayechukua nafasi ya marehemu ,Mambo yalikuwa siyo mambo tena mwenye nguvu ndiyo atakaechukua nafasi hiyo mnyonge itabidi akae pembeni hicho ndicho kilichofanyika .